Matthew 8

1Wakati Yesu aliposhuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata. 2Tazama, mkoma alikuja na kusujudu mbele yake, akasema, “Bwana, ikiwa uko tayari, unaweza kunifanya niwe safi”. 3Yesu akanyoosha mkono wake na kumgusa, akasema, “Niko tayari. Uwe msafi.” Hapo hapo alitakaswa ukoma wake.

4Yesu akamwambia, “Angalia kwamba usiseme kwa mtu yeyote. Shika njia yako, na jioneshe mwenyewe kwa kuhani na utoe zawadi ambayo Musa aliagiza, kwa ajili ya ushuhuda kwao”

5Wakati Yesu alipofika Kapernaumu, Jemedari akaja kwake akamuuliza 6akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza na ana maumivu ya kutisha.” 7Yesu akamwambia, “Nitakuja na kumponya”.

8Jemedari akajibu na kumwambia, “Bwana, mimi si wathamani hata uje na kuingia ndani ya dari yangu, sema neno tu na mtumishi wangu ataponywa. 9Kwa kuwa mimi pia ni mtu niliye na mamlaka, na ninao askari walio chini yangu. Nikisema kwa huyu “Nenda’ na huenda, na kwa mwingine ‘Njoo’ na yeye huja, na kwa mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ na yeye anafanya hivyo” 10Wakati Yesu aliposikia haya, alishangazwa na kuwaambia wale waliokuwa wakimfuata, “Kweli ninawaambia, Sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu katika Israel.

11Ninawambieni, wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, wataketi katika meza pamoja na Abrahimu, Isaka, na Yakobo, katika ufame wa mbinguni. 12Lakini watoto wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno.” 13Yesu akamwambia Jemadari, “Nenda! Kama ulivyokwisha amini, na itendeke hivyo kwako”. Na mtumishi aliponywa katika saa hiyo.

14Wakati Yesu alipofika kwenye nyumba ya Petro, alimwona mama mkwe wake na Petro amelala akiwa mgonjwa wa homa. 15Yesu akamgusa mkono wake, na homa yake ikamwacha. kisha akaamka akaanza kumhudumia.

16Na ilipofika jioni, watu wakamletea Yesu wengi waliotawaliwa na pepo. Akawafukuza pepo na wale walio wagonjwa akawaponya. 17Kwa jinsi hii yalitimia yale yaliyo kwisha kunenwa na Isaya nabii, “Yeye mwenyewe alichukua magonjwa yetu na alibeba maradhi yetu”

18Kisha Yesu alipoliona kusanyiko limemzunguka, alitoa maelekezo ya kwenda upande mwingine wa Bahari ya Galilaya. 19Kisha mwandishi akaja kwake na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata popote utakapoenda.” 20Yesu akamwambia, “Mbweha wana mashimo, na ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana sehemu ya kulaza kichwa chake.”

21Mwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu.” 22Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, na uwaache wafu wazike wafu wao.”

23Yesu alipoingia kwenye mtumbwi, wanafunzi wake wakamfuata mtumbwini. 24Tazama, ikainuka dhoruba kuu juu ya bahari, kiasi kwamba mtumbwi ulifunikwa na mawimbi. Lakini Yesu alikuwa amelala. 25Wanafunzi wakaja kwake na kumwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe sisi, tunaelekea kufa!”

26Yesu akawaambia, “kwa nini mnaogopa, ninyi wenye imani ndogo?” Ndipo akaamka na kuukemea upepo na bahari. Kisha kukawa na utulivu mkuu, 27wanaume wakashikwa na mshangao wakasema, “Huyu mtu niwa namna gani, kwamba hata pepo na bahari vinamtii yeye?”

28Wakati Yesu alipokuwa amekuja upande mwingine wa nchi ya Magadala, wanaume wawili waliotawaliwa na pepo walikutana naye. Walikuwa wakitokea makaburini na walikuwa wakifanya vurugu sana, kiasi kwamba hakuna msafiri angeweza kupita njia ile. 29Tazama, walipaza sauti na kusema, “Tuna nini cha kufanya kwako, mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kufika?”

30Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likichunga, hapakuwa mbali sana walipokuwa, 31pepo waliendelea kulalamika kwa Yesu na kusema. “Ikiwa utatuamuru kutoka, tupeleke kwenye kundi la nguruwe.” 32Yesu akawaambia, “Nendeni!” Pepo wakawatoka na kwenda kwa nguruwe. Na tazama, kundi lote likashuka kutoka mlimani kuteremkia baharini na lote likafia majini.

33Wanaume waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia. Na walipoenda mjini wakaelezea kila kitu, hususani kilichotokea kwa wanaume waliotawaliwa na mapepo. Tazama, mji mzima ukaja kukutana na Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke kwenye mkoa wao.

34

Copyright information for SwaULB